Ahukumiwa kutokunywa pombe miezi 12
Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, imemuachia huru Boniphace Kachila, mkazi wa Kijiji cha Kiyungwe, Kasulu mkoani humo kwa sharti la kutokutenda kosa na kutokunywa pombe ndani ya miezi 12, baada ya Mahakama hiyo kumtia hatiani kwa kosa la kumuuwa baba mkwe wake bila kukusudia.