Vipimo vya Corona kutolewa ndani ya saa 24
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi, ameuagiza uongozi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, kutoa majibu ya sampuli za ugonjwa wa COVID-19 ndani ya saa 24, badala ya saa 72 kwa hospitali zinazopeleka sampuli hizo au kwa wananchi wanaojitokeza kupima kwa ajili ya kusafiri.