Aliyepiga Hat-trick ya Mtibwa aongelea rekodi
Jaffar Kibaya ni jina ambalo kuanzia jana limetawala vinywani mwa wapenda soka nchini baada ya kuifungia klabu yake ya Mtibwa Sugar mabao matatu kwenye ushindi wa 4-0 iliopata dhidi ya Northen Dynamo ya Ushelisheli kwenye kombe la shirikisho barani Afrika.