Kodi ni muhimu kwa maendeleo - naibu waziri Malima
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi nchini Tanzania Mhe. Adam Malima amesema hakuna nchi inayoendeshwa bila wananchi wake kulipa kodi hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuelewa kwamba maendeleo ya nchi
yanapatikana kutokana na ulipaji kodi.