Alizaliwa mnamo mwaka 1977 katika mkoa wa Ruvuma wilaya ya Tunduru. Alisoma na kumalizia elimu yake ya msingi akiwa huko. Rasmi alijiingiza katika fani ya muziki mwanzoni mwa miaka ya 1990 akiwa kama mcheza show katika kumbi mbali mbali za burudani huko na baadae kuhamia katika jiji la Dar-es-salaam huku akiendeleza kipaji alichokua nacho cha kucheza miziki tofauti tofauti kipindi hicho ikijulikana kama breakdance.

Ni kiongozi wa wacheza shoo katika bendi ya Extra Bongo na ni miongoni mwa wanenguaji mahiri na waliodumu katika fani hiyo kwa miaka mingi ambapo amekua mkufunzi na kiongozi wa wachezaji katika bendi ya Twanga Pepeta kwa miaka zaidi ya 10. Nyamwela amefungua chuo cha sanaa kinachofundisha taaluma mbalimbali zinazohusiana na ngoma na nyimbo za asili, ili kukuza utamaduni wa Tanzania.