
Wakizungumza na East Africa Radio jijini Dar es salaam, baadhi ya madereva hao wamesema hali ya maisha sasa inakuwa ngumu kwa upande wao tofauti na ilivyokuwa hapo awali wakati kituo hicho kilivyokuwepo.
Wameiomba serikali na halmashauri ya manispaa ya Kinondoni kuangalia uwezekano wa kuyaruhusu mabasi ya daladala yanayopita katika eneo hilo la kituo cha zamani cha Mwenge kushusha abiria kutokana na sasa kutorohusiwa hata kuwashusha.