Tuesday , 13th Dec , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Ngusa Dismas Samike kuwa Mnikulu Ofisi ya Rais, Ikulu (Comptroller State House - CSH).

Bw. Ngusa Dismas Samike

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Ngusa Dismas Samike umeanza leo tarehe 13 Desemba, 2016.

Kabla ya Uteuzi huo Bw. Ngusa Dismas Samike alikuwa akikaimu nafasi hiyo.