Monday , 12th Dec , 2016

Watanzania wametakiwa kushirikiana na vyombo vya usalama katika kutoa taarifa juu ya matukio ya kihalifu na yanayohatarisha ya amani ya nchi ili kuendelea kuiweka nchi katika hali ya usalama na amani.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

 

Akizungumza katika sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W yaliyofanyika kitaifa mkoani Singida Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema matukio ya hivi karibuni ya kuuawa kwa watu serikali haitavumilia na itaendelea kupambana na wahalifu hao.

Mhe. Majaliwa amesema kumekuwepo kwa vikundi vingi vya uhalifu vikiwemo vikundi vya kigaidi, vinavyohatarisha amani ya nchi hivyo watanzania hawana budi kushirikiana na vyombo hivyo katika kutoa taarifa mapema ili kudhibiti hali hiyo.

Katika hatua nyingine Waziri Majaliwa amewataka askari wa jeshi la polisi wanaotuhumiwa kuwasingizia raia kesi waache mara moja na pindi watakapobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria juu ya matukio hayo.