
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania, Pereira Ame Silima.
Akizungumza leo Jijini Arusha na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wanaoshugulika na masuala ya mitandao, kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika na Duniani, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima amesema hatua hizo ni moja ya kulenga kudhibiti uhalifu wa kimitandao.
Amesema uhalifu ni mkubwa sana na hasa katika mabenki na wizi wa kitaarifa maeneo mbalimbali ya makampuni, hivyo bila kushirikiana na nchi zilizopiga hatua kama Marekani na Ulaya, ili kubadilishana uzoefu, tutakuwa tunajidanganya, ndio sababu washirikishwa.
Silima amesema anaamini kupitia mkutano huo utawezesha kujengea uwezo vyombo vinavyoshughulika na masuala ya mitandao, kwa kupata mbinu mpya za kukabiliana na tatizo hilo.
Amesema ili nchi iweze kufanikiwa ni lazima kuwe na ulinzi wa kutosha katika mitandao, ili wananchi wake wasikumbane na shida.
Aidha amesema kabla ya mafunzo hayo uwezo kwa jeshi la polisi jinsi ya kukabiliana na uhalifu huo, ulikuwa mdogo na wadau wa mawasiliano ila baada ya kupata uzoefu wa nchi zingine wataimarika.
Naye Rais wa Taasisi ya Kimataifa inayoshughulika na masuala ya IT (ISACA), Boniface Kanemba, amesema kupitia taasisi hiyo, wameamua kushirikisha nchi kama Marekani , sababu wao wamepiga hatua katika udhibiti wa uhalifu wa kimitandao kwa kuwa wana uzoefu w amuda mrefu.