Monday , 5th Sep , 2016

Zaidi ya vijana 350 wamekutana jijini Dar es Salaam kutoa mapendekezo yatakayo tumika katika nchi za Afrika pamoja na kwa watunga sera na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na kujiendeleza kiuchumi.

Baadhi ya wahitimu wa moja ya chuo nchini, ambao wengi wao huwaza kuajiriwa baada ya masomo.

Licha ya Tanzania kuonekana inakuwa kiuchumi lakini hali ya vijana wake bado ni mbaya katika uwezo wa kujiajiri kama anavyosema Nesia Mahenge ambaye ni Mwenyekiti wa Kongamano la Vijana Viongozi Barani Afrika, ambapo amesema nchi za Afrika ni lazima ziweke mikakati na mipango madhubuti inayoendana na mbinu za kisasa za kupambana na ukosefu wa ajira.

Mratibu Mkuu wa Kongamano hilo Bi. Margareth Maganga amesema pamoja na kuzitaka nchi za Afrika kuweka mikakati madhubuti za kuwawezesha vijana wake kiuchumi bado ipo haja ya vijana wenyewe kutumia fursa zilizopo katika kujiajiri hasa utatuzi wa changamoto mbalimbali.