Tuesday , 13th Dec , 2016

Serikali imesema viwanda zaidi ya 1500 vimeshajengwa tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani na kwamba kinachotakiwa sasa ni kwa wazalishaji kutafuta taarifa muhimu zinazohusu masoko na taratibu kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda

Charles Mwijage - Wazir wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji

 

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema hayo leo muda mfupi baada ya kuzindua kitabu kinachotoa maelekezo ya jinsi ya kufikia masoko ya bidhaa nje ya nchi, kitabu kilichoandikwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF kwa msaada wa shirika linalojihusisha na uboreshaji mazingira ya biashara kwa nchi za Afrika Mashariki la TradeMark East Africa.

Kauli ya Waziri Mwijage imeungwa mkono na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Louis Accaro ambaye amesema TPSF inajivunia kuwa sehemu ya mdau muhimu katika kampeni ya ujenzi wa viwanda ambapo kila mahali nchini hivi sasa kauli inayozungumziwa ni viwanda viwanda.

Kwa upande wake mwakilishi wa Trade Mark East Africa Bw. Elibariki Shami akiahidi kuwa taasisi yao itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali na wadau wengine wa maendeleo za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kupitia ufadhili katika miradi mbalimbali ya miundombinu ya kiuwekezaji.