Peter Serukamba, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba alipokuwa akitoa marejesho kwa waandishi wa habari mara baada ya kukutana na wadau mbalimbali wa habari nchini kujadili na kupata maoni kutoka kwa wadau hao kuhusu muswada huo.
“Nawapa wadau wiki moja wawe wameleta maoni yao kwa maandishi yaani mpaka Jumatano ya wiki ijayo wawe wameyawasilisha kwa Kamati,” alisisitiza Mhe. Serukamba.
Mhe. Serukamba ameongeza kuwa mchakato wa kuunda sheria unashirikisha wadau husika kwa kuleta maoni juu ya muswada husika na maoni yao yanasaidia katika kutengeneza sheria iliyo nzuri kwa ajili ya tasnia ya habari na maendeleo yake kwa ujumla.
Amesisitiza kuwa anaamini kwa muda ambao kamati imetoa kwa wadau kuwasilisha maoni yao kwa kamati watakuwa wamewasilisha maoni kwa wakati ili kamati iyapitie kabla ya kupelekwa kwa Spika wa Bunge na kuanza kujadiliwa Bungeni.