atibu Mkuu wa Sekta ya Mifugo kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Marry Mashingo
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Sekta ya Mifugo kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Marry Mashingo amesema endapo wakulima wakijiweka kwenye vikundi kuimairisha ufugaji wa kisasa wataweza kuiomboa nchi kupitia sekta ya viwanda.
Dkt. Mashingo amesema kuwa mazao ya mifugo ambayo yanaweza kuleta tija kupitia mapinduzi ya viwanda ni pamoja na Maziwa, Ngozi na nyama ambapo kwa kiasi kikubwa vina soko kubwa ndani na nje ya nchi.
Katibu Mkuu huyo amesema kuwa kwa sasa wameanza kuwekeza kwenye utoaji wa elimu wa ufugaji bora na wenye tija kwa wafugaji ingawa kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya utoaji wa rushwa kwa baadhi ya wafugaji kwa baadhi ya viongozi wa vijiji hali inayosababisha migogoro.
Dkt. Mashingo amesema endapo wafugaji hao wangeweza kuwekeza fedha zao katika kutengeneza miundombinu ikiwemo ya maji wasingepata tabu ya kupata maeneo ya Malisho wakati wa kiangazi hali inayosababisha kuhama toka sehemu moja kwenda nyingine na kusababisha migogoro baina yao na wakulima.