Monday , 9th Mar , 2015

Pambano la kimataifa kati ya Bondia kutoka Tanzania Mohamed Matumla na Bondia kutoka China Wang Xin Hua linatarajia kufanyika Machi 27 mwaka huu Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambalo litarushwa moja kwa moja na kituo cha East Africa.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Muandaaji wa kimataifa Jay Msangi amesema pambano hili litakuwa nila WBF World Tittle Eliminator ambapo Bondia atakayeshinda pambano hili ataweza kushiriki pambano la Ubingwa wa Dunia huku Rais wa shirikisho la ngumi duniani WBF Howard Goiberg anatarajia kuwasili nchini Machi 21 mwaka huu kwa ajili ya kuhudhuria pambano hilo.

Msangi amesema, Bondia Wang Xin Hua kutoka nchini China anatakiwa kuwasili nchini Machi 21 mwaka huu ili nkujiandaa kwa ajili ya pambano hilo linalotarajiwa kusindikizwa na Bingwa wa Kick Boxing Japhet Kaseba akipanda Ulingoni kupambana na mada Maugo katika pambano la Raundi 12 la kuwania Ubingwa wa UBO na Mkanda wa Bingwa Tanzania wa Shirikisho la Ngumi Tanzania PST.

Pambano hilo pia litasindikizwa na Pambano la kumaliza Ubishi kati ya bondia Thomas Mashali na Karama Nyilawila huku Bondia kutoka Tanzania Ashras Suleiman akipanda kupambana na Bondia kutoka Nchini Marekani Joseph Rabotte katika Pambano la Heavy Weight.

Msangi amesema, katika Pambano hilo wameamua kumchagua Matumla kupambana na Bondi kutoka nchini China kutokana na kiwango anachokionyesha Ulingoni pamoja na kufuata Sheria za Ngumi.