Akizungumza na East Africa Radio Kaijage amesema, mechi moja waliyoipata ilikuwa ni ya majaribio na alitamani kupata mechi nyingine ya majaribio ili kukipima kikosi chake baada ya kukifanyia marekebisho.
Kaijage amesema, anaendelea kuyafanyia kazi mapungufu aliyoyaona katika mechi ya kirafiki ili kujihakikishia kikosi chake kinakuwa katika hali nzuri ya kimchezo katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba nne mwaka huu.