Friday , 13th May , 2016

Wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika soko la Sinza Afrika sana wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko na yale yanayoambukizwa kwa njia ya haja ndogo kufuatia soko hilo kukosa maji na kusababisha hali ya choo sokoni hapo kutishia afya.

Wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika soko la Sinza Africa sana wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko na yale yanayoambukizwa kwa njia ya haja ndogo kufuatia soko hilo kukosa maji na kusababisha hali ya choo sokoni hapo kutishia afya za watumiaji.

Akiongea na East Africa Television mwenyekiti wa soko hilo Ashraf Msigiti amesema kuwa choo hiko hakijaunganishwa na system ya maji machafu hali inayowapelekea kila mwezi kulazimika kuagiza gari la kunyonya uchafu na kwa kipindi wanachokosa fedha ya kuagiza gari vyoo hivyo hujaa na kusababisha usumbufu mkubwa..

Aidha uongozi wa soko hilo umeshaandika barua mara kadhhaa kwa uongozi wa Manispaa kwaajili ya kuomba kufanyiwa marekebisho lakini badala ya kufanyiwa marekebisho waliletewa mtu wa kukusanya mapato ya chooilihali choo hiko hakipo katika hali nzuri, hivyo wanauomba uongozi wa Manispaa kufanyia marekebisho choo hiko na kuweka miundombinu ya maji.

Kwa upande wake mfanyabiashyara Devotha Shayo amesema kuwa vyoo ni vichafu na haviridhishi hivyo wanapata wakati mgumu sana katika kutafuta sehemu ya kujihifadhi.