Thursday , 20th Oct , 2016

Wamiliki wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa nchini wametakiwa kutumia mfumo wa 'Kaizen' uliobuniwa na taifa la Japan,  unaotumika kuongeza tija, ubora za bidhaa pamoja na kupunguza hasara katika uzalishaji viwandani.

Mkurugenzi Mkuu wa Ando, Bw. Ado Maimu

 

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mheshimiwa Charles Mwijage, ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam, katika hafla ya utoaji zawadi kwa makampuni na viwanda vilivyofanya vizuri katika utumiaji wa mfumo huo, hatua inayoonesha mwelekeo mwema wa kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Baadhi ya washindi wamezungumzia jinsi Kaizen ilivyosaidia kuongeza tija na uzalishaji katika viwanda vyao ambapo mmoja wa washindi hao ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha mabati cha Ando Bw. Ado Maimu ambaye amesema tangu waanze kutumia Kaizen hakuna bidhaa zinazorudishwa kutoka kwa wateja kutokana na ubora hafifu.