Monday , 2nd Dec , 2019

Thamani ya Mauzo ya Hisa sokoni kwa mwaka 2019, imeongezeka karibu mara mbili zaidi ya mwaka jana, ambapo kwa sasa imefikia bilioni 606.30, ukilinganisha na mauzo ya mwaka 2018 ambayo yalikuwa bilioni 208.36.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 2, 2019, na Meneja Miradi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Emmanuel Nyalali, wakati akitoa ripoti ya soko kwa juma lililoishia Novemba 29, 2019.

Aidha Nyalali amesema kuwa mpaka sasa thamani ya hatifungani zilizoorodheshwa sokoni hapo, zimefikia trilioni 10.40, ambazo ni sawa na hatifungani za Serikali zenye thamani ya Shilingi trilioni 10.225, na hatifungani zilizotolewa na taasisi za kifedha za Tanzania na za Kikanda zenye thamani ya Shilingi bilioni 176.