Friday , 13th Dec , 2019

Muigizaji Mwijaku amefunguka na kusema suala la Nandy kutaka kuwa mke wa mtu ni jambo jema na amejibashiria jambo zuri  katika maisha yake.

Kushoto kwenye picha ni Mwijaku, kulia ni Nandy.

Siku ya Novemba 18, 2019 kwenye ukurasa wa mtandao wa Instagram, Nandy alipost picha na kuandika anaenda kuwa mke wa mtu, jambo ambalo lilifanya watu wahisi amepata mchumba na anajipanga kwa ajili ya kufunga ndoa.

"Nimeishi na Nandy ni miongoni mwa watu waliofundwa na wakafundika ni Mke halisi, hakuna kitu ambacho kinaumiza wanawake kama kuendelea kuwa 'single' na kutokuwa na mtu wa moja kwa moja, kwahiyo mtu kama Nandy kuanza kupambana kusema anataka kuwa mke wa mtu ni jambo zuri" ameeleza Mwijaku.

Aidha Mwijaku ameongeza kuwa, "Unajua unatakiwa ujibashirie jambo zuri ndiyo mambo yanaenda, yeye anajibashiria ndoa ili maisha yake yawe mazuri, sijajua ni nani atakae kuwa naye ila atatuweka wazi maana Nandy naye siku hizi amekuwa msiri sana kwenye mahusiano yake na amekuwa msafi".