Thursday , 16th Jan , 2020

Taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari nchini Uingereza leo zinasema kuwa mshambuliaji wa Taifa Stars na klabu ya Genk, Mbwana Samatta yukom mbioni kusajiliwa na klabu ya Aston Villa.

Mbwana Samatta

Kwa mujibu wa chanzo cha Daily Star, Aston Villa inakaribia kumsajili Samatta kwa kiasi cha Pauni milioni 8.5, ambapo hii leo amefanya mazoezi na timu yake lakini anatarajiwa kusafiri hadi nchini Uingereza kukamilisha dili hilo.

Samatta (27) ambaye yupo katika msimu wake wa nne katika klabu yake Genk, amekataa ofa mbalimbali kutoka klabu za Mashariki ya Kati akishinikiza uhamisho wa kwenda ligi kuu nchini Uingereza ambako ndio ndoto yake ilipo.

Bosi wa Aston Villa, Dean Smith amethibitisha kuwa klabu inahitaji kuongeza nguvu ya kikosi baada ya changamoto walizopata katika mzunguko wa kwanza, "tunalifanyia kazi hilo muda wote, ninafikiri tutakamilisha kabla ya Jumapili", alisema wiki iliyopita.

Aston Villa iko katika nafasi ya 18 ya msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza kwa sasa na inahitaji mshambuliaji wa kati baada ya kuumia kwa mshambuliaji wake, Wesley