Monday , 20th Jan , 2020

Msanii wa filamu Dorah, amepiga stori na EATV & EA Radio Digital, ambapo amefunguka kuhusu mastaa kuogopa kupata watoto kwa kuhofia kupoteza mvuto, na mahusiano gani anayafurahia zaidi kati ya mwanaume aliyemzidi umri au yeye kumzidi.

Picha ya msanii wa filamu Dorah

Akizungumzia juu ya mastaa kuogopa kujifungua au kuingia kwenye uzazi kwa kuhofia kuharibu muonekano wao, Dorah amesema kuwa.

"Ni wewe mwenyewe tu utakavyojiweka, unaweza ukajifungua na ukaendelea vizuri, halafu unaweza ukajifungua vilevile ila ukaharibu, kwahiyo ni jinsi tu utakavyojiweka na utakavyoandaa mazingira na itakavyokuwa, kwani mastaa wangapi wanajifungua na maisha yao yanaendelea kama kawaida ni jinsi ya kuchagua tu" ameeleza Dorah.

Aidha kuhusu suala la kuwa kwenye mahusiano na mwanaume aliyemzidi umri au yeye ndiyo kumzidi umri Dorah amesema, "Inategemea na mwanaume gani, mimi siwezi kuwa kwenye mahusiano ili mradi tu mtu amenizidi umri au nimemzidi, naweza nikawa na yeyote hapo na nikafurahia ila ninachoangalia ni upendo tu".