Monday , 20th Jan , 2020

Mrembo na msanii Miss Bella, amesema Tanzania nzima hakuna mwanamke mzuri na wa gharama kumshinda yeye, pia amewapa somo wasanii wote ambao hawatoki bila kufanya urembo usoni yaani kupaka make up.

Picha ya Miss Bella

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Miss Bella, amesema wanawake wengi wanapata shida wanapopaka make up usoni, kutokana na hali ya hewa ya sasa.

"Mimi naweza nisifanye make up na nikafanya mahojiano ya TV, wao hawawezi lazima wafanye hivyo, naongea ukweli sasa hivi hali ya hewa ni joto kali, unatakiwa ufanye make up labda ukiwa unarekodi video au tangazo ukimaliza futa kuwa wa kawaida tu, maana kila kitu lazima wafanye make up hata wakati wa kupika hadi ngozi inachoka" amesema Miss Bella.

Aidha Miss Bella amesema wanawake ambao wanavaa shanga kiunoni, ndiyo wana gharama zaidi duniani kote na Tanzania nzima hakuna mwanamke mzuri kama yeye, kuanzia BongoMovie au BongoFleva hakuna anayemuweza.