Wednesday , 22nd Jan , 2020

Mamalaka ya hali ya hewa nchini  (TMA), imetoa tahadhari ya uwezekano wa uwepo wa mvua kubwa kwa Mikoa mitano nchini Tanzania, ikiwemo Mtwara, Lindi, Pwani, Ruvuma na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.

Picha: Mvua ikinyesha

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo imeeleza kuwa mvua hizo zitanyesha kuanzia Januari 21 hadi Januari 25, 2020.

"Tunatoa tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa kwa baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Lindi na Mtwara, athari zinazoweza kujitokeza ni kuathirika kwa shughuli za uvuvi, ucheleweshwaji wa usafiri pamoja na kuanguka kwa majani na matawi madogomadogo ya miti." imeeleza taarifa hiyo.

Aidha mamlaka hiyo imewataka wananchi wa Mikoa hiyo, kuzingatia tahadhari iliyotolewa na wajiandae.