Wednesday , 22nd Jan , 2020

Kinda wa Azam FC, Tepsi Evance amesafiri kuelekea Ufaransa kwaajili ya majaribio ya kucheza soka katika klabu ya Nantes inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo. 

Tepsi Evance

Tepsi ambaye amechezea timu mbalimbali za taifa za vijana chini ya miaka 17 na 20, ameondoka nchini leo Jumatano, Januari 22 kuelekea nchini humo.

Kinda huyo alisajiliwa na Azam FC akitokea shule ya Jitegemee ambapo alilelewa kwa kipindi chote mpaka sasa alipopata nafasi hiyo kwenda kufanya majaribio Ufaranza.

Huyo ni mchezaji wa tatu kijana zaidi kwenda barani Ulaya, baada ya Ally Ng'anzi ambaye anacheza katika klabu ya Minesota United ya Marekani pamoja na Kelvin John anayelelewa katika kituo cha soka Jijini Leicester City, huku kukiwa na matarajio ya kusajiliwa na KRC Genk atakapofikisha umri wa miaka 18.

Klabu ya Nantes inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligue 1, ikiwa na pointi 32 katika michezo 20 iliyocheza mpaka sasa.