Wednesday , 22nd Jan , 2020

Msanii wa kundi la B.O.B Micharazo Beka Title,  amesema yupo tayari kwa vita muda wowote kuanzia sasa kwa sababu Nyandu Tozzy na Mr Blue wanawaongelea vibaya kwenye mahojiano yao, pia hawajawasaidia walipoachia kazi yao mpya.

Kuanzia upande wa kushoto pichani Beka Title, kati Nyandu Tozzy na kulia ni Mr Blue

Kupitia eNewz ya East Africa TV, Beka Title amesema, Mr Blue na Nyandu Tozzy, wamepaniki kwa kuona kazi yao imefanya vizuri kuliko ngoma zao wao na lolote litakalotokea kwenye kundi lao yupo tayari.

"Nimeona mahojiano ya Nyandu mengi  ana-diss anatuambia sisi watoto wadogo, tulivyotoa wimbo wa sio kinyonge nilitegemea yeye na Mr Blue watasapoti lakini wamekunja, wameweka roho mbaya kama wamefanya hivyo sawa kama mbwai na iwe mbwai tu, mwisho wa siku haya ni maisha kila mtu anatafuta riziki" ameeleza Beka Title.

Beka Title ameongeza kusema "Wale wamepaniki ngoma yetu imehit sana, tumefanya show kadhaa wao zao zimefeli kwa hiyo wamekuwa kama wanatapatapa, sipendi mtu ambaye hataki kuona wenzake wanafanikiwa ndiyo wale jamaa walivyo na kama mtu anataka vita na mimi nipo tayari muda wowote".

Kumekuwa kuna migogoro ambayo inaendelea kwenye  kundi la B.O.B Micharazo, ambapo Mr Blue amesema kuna baadhi ya wasanii wamewapunguza kwenye kundi hilo kutokana na utovu wa nidhamu.