Saturday , 23rd May , 2020

Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali, ambaye alikuwa mwanachama wa CHADEMA kabla ya kutangaza kuhama hivi karibuni, amejitokeza na kueleza mambo mengi kuhusu Chama hicho.

Peter Lijualikali

Akiongea na waandishi wa habari leo Mei 23, 2020 amesema chama hicho kina matumizi mabaya ya fedha huku akieleza kuwa hata ripoti ya CAG inaeleza juu ya mapungufu hayo.

Mengine ambayo ameeleza Lijualikali ni juu ya matumizi ya fedha ambazo walikatwa ili zitumike kwaajili ya uchaguzi mkuu wa 2020, ambapo ameweka wazi kuwa zaidi ya Mil 400 zilitolewa kwenye akaunti ili kwenda kumtibu Tundu Lissu alipopigwa risasi mwaka 2017.

'Tumetoa pesa zetu za mfukoni na kukatwa shilingi laki tano lakini Mwenyekiti Freeman Mbowe yeye ndio ana saini ya akaunti zote hivyo amekuwa akitoa pesa bila hata wengine kuhusishwa'', - Lijualikali.

Zaidi msikilize hapo chini akieleza