Sunday , 24th May , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, amewataka viongozi wa dini wilayani Gairo kuiombea Wilaya hiyo na Taifa, dhidi ya ugonjwa wa Corona, kwa kile alichokidai kuwepo kwa baadhi ya wanasiasa wakidai kuna Watanzania Milioni 1 watafariki kwa ugonjwa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Seriel Mchembe ameyasema hayo kwenye ibada maalumu ambayo imeyakutanisha makanisa yote wilayani hapa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kutokana na kupungua kwa maambukizi ya virusi vya corona.

"Kuna mwanasiasa aliniambia Tanzania kuna watu Milioni 1 watafariki, nikamwambia utaanza kufariki wewe kabla hata Sisimizi hajafariki" amesema DC Mchembe

Kwa upande wao baadhi ya waumini wamesema kuwa wataendelea kufanya kazi bila kuogopa  chochote huku wakiwashangaa watu wasioitakia mema nchi ya Tanzania dhidi ya virusi vya corona.

Tazama video kamili hapo chini