Tuesday , 26th May , 2020

Mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Rwanda Meddie Kagere, ameweka wazi kuwa yupo njiani kurejea Tanzania akitokea kwao Rwanda.

Meddie Kagere

Kagere amebainisha hilo kwenye mahojiano na East Africa Television/ East Africa Radio, ambapo amesema anaondoka Rwanda mchana wa leo Mei 26, 2020 na atafika Tanzania jioni.

''Naingia leo tayari kwa kuendelea na maandalizi ya kumalizia msimu wa ligi kuu na timu yangu, kwasasa ndo nataka kuanza safari kwahiyo nitafika huko jioni'', amesema.

Simba imeshaweka wazi kuwa mazoezi yataanza kesho Mei 26, 2020 kwenye uwanja wao wa Mo Arena uliopo Bunju Dar es salaam.

Licha ya timu yake kuongoza msimamo wa ligi kuu, lakini Kagere ndio kinara wa magoli msimu huu akiwa amefunga magoli 19.