Msanii Billnass akiwa ukweni kwa familia ya Nandy
Kupitia picha ambazo wamepost katika kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram inaonyesha kuwa Nandy amempeleka Billnass katika familia yake kwa kumkutanisha na Baba, Babu na bibi yake.
"Niko na mwenye jina lake Nandera bibi yangu kipenzi na babu yangu kipenzi upareni kwetu, tuko na baba mzaa vyema na watoto wake Charles Mfinanga" ameandika Nandy
Aidha kwa upande wa msanii Billnass ameandika kuwa "Wapare ni watu wakarimu sana, na wenye upendo, sitamani kuondoka upareni, Usangi nimepapenda sana"

