Tuesday , 14th Jul , 2020

Waasisi wa klabu ya soka ya Stand United ya Shinyanga wameandaa sherehe ya kusherehekea kushuka daraja kwa timu hiyo kutoka ligi daraja la Kwanza.

Kikosi cha Stand United katika picha ya pamoja(Pichani)

Akizungumza na kipindi cha michezo cha East Africa Radio,muasisi na muanzilishi wa klabu ya Stand United ambaye pia ni mjumbe wa Stand Kampuni,Mohamed Salehe amesema matokeo ya kushuka daraja kwa timu hiyo kwa mikono miwili,kwa kuwa matokeo ya dhuluma dhidi yao yameanza kuonekana.
 

Salehe amesema Mungu anawaonyesha wananchi wa Shinyanga,kuwa timu hiyo haikua ya wananchi wa mkoa huo,bali ilikua ni timu ya watu wa Stand,hivyo waliohusika kuwapindua ndio wamepeleka mabaya haya yanayowatokea.
 

Kiongozi huyo ameongeza kuwa siku ya Ijumaa watachinja Ng'ombe,Mbuzi na Kondoo katika kuherehekea kushuka kwa timu hiyo,na pia watahakikisha wanakwenda bega kwa bega hadi wahakikishe timu hiyo inapotea kwenye ramani ya soka na ibaki kuwa historia.
 

Mnamo mwaka 2016, kampuni ya uchimbaji wa madini ACACIA ambayo iliwekeza kiasi cha Bilioni 2.4 ilitoa totisi ya miezi mitatu kuwa ingevunja mkataba wa udhamini kutokana na mgogoro uliotokana na pande mbili kuvutana katika uongozi.