Wednesday , 15th Jul , 2020

Mshambuliaji wa timu ya Manchester United Marcus Rashford anatarajiwa kutunukiwa shahada ya heshima na chuo kikuu cha Manchester.

Marcus Rashford akishangilia moja ya bao aliloifungia klabu yake.

Rashford   anatarajiwa kutunikiwa  tuzo hiyo kutokana na mchango wake kwa jamii na  mafanikio kwenye soka hivyo kuingia katika  rekodi  kutokana na  umri  wake mdogo.

Tuzo hiyo inatokana na kampeni yake dhidi ya umasikini , ikiwemo mapendekezo yake kwa serikali na taasisi mbalimbali kuwasaidia vijana mashuleni wanaotoka katika familia duni kwa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula.

Marcus Rashford ni zao la timu ya Manchester United ambayo alijiunga nayo akiwa mdogo na hatimaye kupandishwa timu ya wakubwa , na kwa sasa anatoa mchango mkubwa sana katika timu hiyo.