Wednesday , 15th Jul , 2020

Kutoka kwenye kamati ya hamasa ya timu ya Yanga Jimmy Kindoki kwa mara ya kwanza leo amekutana na shabiki maarufu wa klabu hiyo, ambaye anafahamika kwa jina la utopolo na wamefanikiwa kumaliza tofauti zao.

Kutoka upande wa kushoto ni Utopolo kulia ni Jimmy Kindoki

Wawili hao walikuwa hawana maelewano mazuri kwa sababu Jimmy Kindoki, alikuwa anadai jina la utopolo linaharibu brand ya timu ya Yanga, huku Utopolo akiamini kufanyiwa fitina na kutumiwa watu wa kumpiga kutoka kwa Kindoki.

Mara baada ya kukutana kwao wameonekana kumaliza tofauti zao, kuungana na kuwekana sawa kwa njia ya kutengeneza mikakati mipya ndani ya Klabu ya Yanga na kuzidi kuleta upinzani kwa watani wao wa jadi Simba.

"Kusema ukweli nimefurahi kukutana na Jimmy Kindoki kwa sababu zile tofauti zitaisha, nisingependa ugomvi wakati tunaisapoti  timu moja, baada ya kuungana Simba atakipata cha mtema kuni watakuwa wamekutana na moto wa gesi tiba kwa mdomo, tutawaunguza vibaya sana, Manara tutamfukia" amesema Utopolo.