Sunday , 2nd Aug , 2020

Staa wa filamu hapa nchini Wema Sepetu amesema kiu yake itaisha endapo atapata mtoto wake, ila kama hajampata itaendelea kumuuma mpaka kifo na hadi pale atakapoingia kaburini bila mtoto.

Msanii wa filamu Wema Sepetu

Wema Sepetu amesema roho yake itakuwa imesuuzika endapo akimshika wa kwake na hapo ndipo atakapoacha kuwajibu wote wanaomshambulia kwamba hajapata mtoto japo yote ni mipango ya Mungu.

"Linapokuja suala la mtoto na mimi, nahisi kiu yangu itaisha pale nitakapomshika wa kwangu na itaendelea kuniuma mpaka nitakapopata wangu, itaniuma mpaka kesho hadi kifo na kama Mungu amenijalia nisipate sawa hamna shida kwa hiyo nitaingia kaburini bila mtoto wangu bado nitaumia" Wema Sepetu 

Zaidi tazama kwenye video hapo chini.