Friday , 7th Aug , 2020

Mbunge wa Rombo aliyemaliza muda wake Joseph Selasini, ameviomba vyama vyote nchini kuhakikisha vinawapokea vijana wote waliohama vyao vyao na kuhamia vyama vingine lakini wakashindwa kwenye kura za maoni kwa kuwa walishaonesha wanao uwezo wa kufanya kazi.

Mbunge wa Rombo aliyemaliza muda wake Joseph Selasini.

Selasini ametoa kauli hiyo hii leo Agosti 7, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi na kuongeza kuwa vijana hao wanapashwa kuwapokea na kisha kuwalea na kuwarekebisha kwenye makosa yao na kuwapa nafasi za uongozi.

"Naviomba vyama vyote, chama changu cha NCCR-Mageuzi, CCM, CHADEMA tusiwatupe vijana, hata vijana ambao walihama kutoka CHADEMA kwenda CCM wakaenda kushindwa kwenye kura za maoni, tunajua vijana wanavyotangatanga hata katika kutafuta uchumba, wanatafuta fursa fungueni milango hao vijana warudi waweze, kufanya kazi ya Watanzania" amesema Selasini.

Mkutano Mkuu wa NCCR-Mageuzi hii leo una ajenda moja mahususi ambayo ni kuchagua na kuwapitisha wapeperusha bendera wa chama hicho katika nafasi yab Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.