Friday , 7th Aug , 2020

Licha ya Serikali kuwezesha mikopo ya yenye masharti nafuu kwa wanawake, vijana na watu walemavu kupitia Halmashauri mbalimbali nchini kuwasaidia vijana kufanya shughuli za ujasiriamali bado tatizo kubwa limetajwa kuwa ni vifungashio vyenye ubora.

Mmoja ya kijana mjasiriamali anayejishughulisha na utengenezaji wa sabuni za mche pamoja na sabuni za maji dawa za kusafishia maliwatoni amesema wanapata wakati mgumu kusafirisha sabuni hizo umbali mrefu kutokana na vifungashio kuwa duni.

Hata hivyo amesisitiza ni vyema vijana wengi wakaacha kuilalamikia serikali na badala yake wajitokeze kujifunza mbinu ya kujisimamia wenyewe katika ujasiriamali ili kukuza vipato vyao.

Kuhusu Sera za Serikali katika biashara na viwanda amesema ni muhimu zikazingatia kuwakuza hasa wafanyabiashara wa ndani ili waweze kuwa na ushindani katika masoko makubwa na wafanyabiashara wanaotoka nje.