Friday , 7th Aug , 2020

Msemaji Mkuu wa wanawake kutoka East Africa Television na East Africa Radio Maryam Kitosi, leo Agosti 7 katika kipindi cha MamaMia kinachoruka East Africa Radio Jumatatu hadi Ijumaa Saa 10:00 Asubuhi hadi 12:00 mchana, ametoa wito kwa mama lishe kuwa na dhamira ya maendeleo.

Maryam Kitosi

Maryam Kitosi amesema anataka kuwaongezea mama lishe thamani yao kupitia kampeni  ya Simama Na Mimi, inayoendeshwa na East Africa Radio, ambapo amewasihi mama lishe kutumia lugha nzuri na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara hiyo ili kumvutia mlaji.

Pia ameongelea suala zima la afya ya Uzazi ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji, ambapo ameshirikiana na mtaalamu Kutoka Tiba na Lishe na kutoa elimu ya namna ambavyo mama anatakiwa kunyonyesha.

“Inashauriwa ndani ya saa moja baada ya mama kujifungua mtoto aanze kunyonya ndani ya muda wa miezi sita na ndipo apewe chakula kingine kama nyongeza hadi atakapotimmiza miaka miwili, kunyonyesha kunajenga mahusiano mazuri katika ya mama na mtoto na inaongeza upendo kati yao’’, amesema mtaalamu kutoka Tiba na lishe.

Pia Kinara huyo alihitimisha kwa kusema wanawake wazingatie miongozo ya afya katika unyonyeshaji ili kujilinda na saratani ya matiti.