Saturday , 8th Aug , 2020

Siku ya Jana Julai 7 ilikuwa weekend ndevu sana hapa kwenye Jiji la Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Abubakar Kunenge kwa sababu kulikuwa na matukio mawili makubwa ya burudani ambapo Rich Mavoko alikuwa anaachia Minitapae yake huku Mzee Yusuph akirudi.

Msanii Mzee Yusuph kushoto, kulia Rich Mavoko

Kwa upande wa Rich Mavoko alikuwa kimya miezi saba bila ya kuachia kazi mpya, kuonekana kwenye shughuli za burudani, mahojiano na kutotumia mtandao wa Instagram jambo ambalo lilizua maswali kwa mashabiki juu ya ukimya wake.

Kwa hiyo siku ya jana alifanikiwa kuachia Minitape yake ambayo inangoma nane huku akiwaalika mastaa kama Jux, Ebitoke, Nedy Music, Mwijaku, Shetta na Barnaba kuhudhuria tukio hilo.

Mzee Yusuph alitangaza kuacha muziki miaka mitano iliyopita ila siku jana ameweza kurudi mjini kwa mara na kutoa nyimbo mpya na kufanya show mbele ya mamia ya watu walijitokeza huku akisema Taarab haijafa bali watu walimiss uwepo wake.