Saturday , 8th Aug , 2020

Leo usiku katika dimba la Camp Nou katika jiji la Barcelona kutapigwa mchezo wa marudiano wa hatua ya kumi na sita bora ya ligi ya mabingwa Ulaya, kati ya wenyeji timu ya Barcelona dhidi ya Napoli kutoakea Italia.

Kama picha inavyoonyesha nahodha wa Barcelona Lionel Messi (kushoto ) na Dries Mertens wa Napoli ( kulia) wote wanatarajiwa kupigania vilabu vyao usiku wa leo.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Stadio San Paulo nchini Italia timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana goli 1-1.

Barcelona wanaingia katika mchezo huo dhidi ya Napoli wakiwa na machungu ya kupoteza ubingwa wa La Liga waliokua wakiushikilia kwa misimu mitatu mfululizo uliochukuliwa na mahasimu wao wakubwa Real Madrid.

Huu ni mchezo muhimu sana kwa klabu ya Barcelona kama watataka kumaliza msimu na medali za ubingwa wowote basi ni lazima waifunge timu ya Napoli.

Katika mchezo wa La Liga Barcelona walipoteza kwa kufugwa (2-1), dhidi ya Osasuna kepteni wa timu hiyo Lionel Messi alikaririwa akisema kama wanataka kuwafunga Napoli ni lazima wawe bora zaidi katika maeneo yote ndani ya Uwanja.

REKODI ZINAIBEBA TIMU YA BARCELONA KATIKA UWANJA WA CAMP NOU

Timu ya mwisho kupata ushindi katika uwanja wa Camp Nou katika mechi yao ya kwanza ya ushindani dhidi ya Barcelona ni Rubin Kazan mwezi wa kumi mwaka 2009 (2-1).

Barcelona imefanikiwa kuvuka katika mechi za 19 za mtoano ambazo timu ya Barcelona ilifanikiwa kutokupoteza mechi za awali walizocheza katika viwanja vya ugenini.

Msimu mmoja tu wa 2002-2003 ambao Barcelona walitolewa katika hatua ya Robo Fainali dhidi ya Juventus mara baada ya kutokupoteza mcheza wao wa kwanza nje ya dimba la Camp Nou ,mechi ya kwanza (1-1) Nchini Italia na mechi ya pili (2-1) Camp Nou nchini Hispania.

Napoli imeshinda mechi moja tu kati ya 10 iliyocheza katika uwanja wa ugenini, (D4 L5), imeshinda ugenini dhidi ya Red Bull Salzburg mwezin wa kumi 2019. Japokua Napoli aijapoteza michezo mitatu ya ugenini msimu ya ligi ya mabingwa balani ulaya (D1 W2).

Lionel Messi amehusika katika goli 11 katika mechi tano za mtoano za ligi ya mabingwa balani ulaya katika uwanja wa Camp Nou (kafunga 8 katengeneza 3) amefunga magoli mawili katika mechi nne kati ya mechi hizo tano zilizopigwa katika dimba la Camp Nou.

Huu ni mchezo wa kwanza wa Barcelona wa ligi ya mabingwa Ulaya katika uwanja wa nyumbani ikiwa chini ya kocha Quique Setien.

Makocha 10 kati ya 11 wa zamani wa Barcelona walishinda michezo yao ya kwanza ya ligi ya mabingwa ulaya katika uwanja wa Camp Nou, ni Luis Van Gaal pekee aliyetoa sare ya (2-2) dhidi ya PSV Eindhoven mwaka 1997.

Barcelona imefuzu katika hatua ya Robo fainali katika misimu 12 mfululizo, mara ya mwisho Barcelona kushindwa kufuzu hatua ya Robo fainali ilikua ni msimu wa 2006-2007 chini ya kocha Frank Rijkaard, hakuna timu nyingine iliyofuzu hatua ya robo fainali ya mara 8 mfululizo zaidi ya Barcelona.

WATAKAOKOSEKANA KATIKA MCHEZO HUO.

Kwa upande wa Barcelona, itawakosa nyota wake Arthur Melo ambaye hayupo kikosini,Sergio Busquets mwenye kadi na na Arturo Vidal wakati kwa Napoli hakuna ripoti yoyote ya majeruhi.