Sunday , 20th Sep , 2020

Mshambuliaji machachari wa Southampton na timu ya taifa ya Uingereza Danny Ings amefunga mabao mengi zaidi katika EPL mwaka huu mabao 12 bao moja nyuma ya mshambuliajia wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah

Kocha wa timu ya Tottenham Hotspurs

Rekodi hiyo ya Ings ameiandika leo baada ya kikosi chake kufungwa mabao 5-2 dhidi ya Tottenham Hotspurs, Raia wa Korea Kusini Heung-Min Son amerudi kambani mara nne huku Harry Kane akirudi kambani mara moja na kutoa pasi nne za mabao.

Hadi sasa pacha ya Heung-min Son na Harry Kane inakuwa ndiyo pacha iliyotengeneza idadi kubwa ya mabao kwa jumla ya mabao 22 EPL tangu muunganiko wao ulipoanza kufanya mwaka 2015.

Ikumbukwe Tottenham tayari imeshakamilisha usajili wa mkopo wa mwaka mmoja kwa aliyekuwa mchezaji wao wa Raia wa Wales Gareth Bale kutoka Real Madrid ambapo awali aliondoka klabuni hapo mwaka 2013.

Ingizo hili jipya kikosini huwenda ukatengeneza utatu mtakatifu zaidi kuwahi kutokea EPL baada ya utatu wa Berbatov, Ronaldo na Rooney waliyotikisa zama za babu Ferguson pale Old Trafford.