
Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere(Mwenye jezi namna 14) akishangilia bao wakati mnyama akiwaadhibu Kagera Sugar msimu ulipita
Simba ambayo kwasasa inakamata nafasi ya tatu katika msimamo wa VPL, wanahitaji ushindi ili kurejesha hali ya kujiamini kabla ya kukabiliana na mtani wake Yanga siku ya Jumamosi mchezo utakaochezwa katika dimba la Benjamin Mkapa.
Kwa upande wa Kagera Sugar, ni timu ambayo haijaanza vyema msimu huu, lakini wamekuwa na kawaida ya kuvisumbua vilabu vikongwe nchini hususan Simba na Yanga.
Takwimu zinaonesha kwamba katika mechi kumi walizokutana katika uwanja wa Mkapa (Zamani Taifa), wameshinda mara tatu, wametoa sare tatu na kupoteza mechi nne.
Kuna kila dalili ambazo zinaonesha kwamba Simba itakuwa na wakati mgumu kukabiliana na Kagera Sugar inayonolewa na kocha Mecky Mexime ambaye kwasasa ndiye aliyedumu katika timu moja kwa muda mrefu kuliko wote waliopo hivi sasa.
Wekundu wa msimbazi watashuka dimbani leo ikiwa inawakosa washambuliaji wake muhimu Meddie Kagere, Chris Mugalu ambao walishaanza kuwasha moto ambao kwasasa ni majeruhi ingawa wameanza mazoezi mepesi lakini wamepata ahueni kwa urejeo wa nahodha wake John Bocco ambaye amerejea na katika mechi iliyopita alipachika mabao mawili dhidi ya Mwadui.
Kagera Sugar inajivunia uwepo wa mshambuliaji wale Yusuph Mhilu aliye katika kiwango cha hali ya juu, akiwa amepachika mabao manne hivi sasa, pia ina mlinzi mwenye uzoefu Ally Mtoni Sonso na David Luhende ambao kwa ujumla wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa wanamkurukumbi hao.
Dakika tisini zitaamua je yupi ataibuka mbabe?