
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile, mkoani Arusha wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wa mkoani humo alipotembelea taasisi za wizara hiyo na kutumia nafasi hiyo kuwaasa wote wenye tabia hizo kwani ni kinyume cha sheria.
Amesema kuwa baadhi ya mafundi simu wasio waaminifu wanatumika kufuta IMEI (International Mobile Equipment Identity) namba za simu za mkononi za wateja wao ili simu hizo ziweze kutumika tena ambacho ni kosa kisheria na serikali itawachukulia hatua kali mafundi watakaobainika kufanya tabia hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa TCRA Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Imelda Salum, ametoa rai kwa wawekezaji wa sekta ndogo ya utangazaji kujenga studio za redio kwenye kanda hiyo kwa kuwa baadhi ya maeneo hayana usikivu kwani kwa kufanya hivyo kutachochea maendeleo ya wananchi kwa kuwa kanda hiyo ina fursa katika sekta ya utalii na hivyo vifaa na huduma za mawasiliano vinatumika ipasavyo.