Tuesday , 13th Apr , 2021

Msanii wa filamu na muziki wa HipHop kwa sasa Rose Ndauka amesema wasanii wa BongoMovie walipendwa sana na mashabiki ndio maana hata wakifanya mambo madogo yanachukuliwa kwa ukubwa.

Msanii wa filamu na muziki Rose Ndauka

Rose Ndauka amesema ujio wao ulikuwa mkubwa na wakati huo hakukuwa na mitandao ya kijamii kama Instagram, WhatsApp wala Facebook ila sio kwamba walikuwa na kashfa au visa vingi.

"BongoMovie tumependwa sana na mashabiki na ujio wetu ulikuwa mkubwa sana, wakati tunatoka kulikuwa hakuna Instagram, Facebook wala WhatsApp ilikuwa ni rahisi kufanya vitu hata vikiwa vidogo ila vinachukuliwa kwa ukubwa kwenye jamii ila haimaanishi kwamba BongoFleva au tasnia zingine hazifanyi visa" ameeleza Rose Ndauka

Aidha msanii huyo ameendelea kusema tatizo hilo la kuandamwa na kashfa nyingi iliwaumiza sana wasanii wa filamu ila anawaomba mashabiki waendelee kuiheshimu kazi hiyo.

Zaidi bonyeza hapa kutazama interview nzima