Friday , 18th Jun , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kwa wanafamilia na Rais wa Zambia Edgar Lungu, kufuatia kifo cha Rais wa Kwanza na Muasisi wa Taifa hilo Kenneth Kaunda, kilichotokea jana Juni 17, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan

Kaunda amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 97, ambapo imeelezwa kwamba mauti yalimfika wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Jeshi ya Maina Soko iliyopo Lusaka, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, ameeleza kuwa Afrika imeondokewa na tunu na itaendelea kumkumbuka kwa yale aliyoyafanya katika nchi yake na Afrika kwa ujumla na kwamba ataendelea kumkumbuka kwa ushauri wake aliokuwa akimpatia wakati akiwa bado ni Rais hata baada ya kustaafu.