Saturday , 19th Jun , 2021

Watu wawili wamepoteza maisha na wengine wanne kujeruhiwa, baada ya duara moja katika mgodi wa dhahabu wa EMJ, uliopo Dutwa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, kuporomoka.

Sehemu ya mitambo katika mgodi huo

Kufuatia ajali hiyo serikali imetangaza kuufunga mgodi huo kwa muda wa siku tatu, ili kupisha ukaguzi wa wataalamu wa madini katika mduara mgodini hapo.

Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, akiwa na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Simiyu, Mhandisi Amini Msuya na maafisa wengine wa serikali, wamefika katika mgodi huo na kutangaza zuio hilo.