Wednesday , 29th Dec , 2021

Mchezo wa ugenini kati Newcastle United dhidi ya Everton uliopangwa kucheza siku ya Decemba 31, umehairishwa kutokana na kuibuka kwa wimbi kubwa la maambukizi ya UVIKO-19 na ongezeko la majeruhi katika kambi ya Newcastle.

Newcastle inajumla ya majeruhi na wagonjwa 19 wa UVIKO-19 hivyo kukifanya kikosi chao kiwe finyu huku washambuliaji wake machachari Callum Wilson na Allan Saint-Maximin kuumia kwenye mchezo wa jana dhidi ya Manchester United uliomalizika kwa Sare.

Kocha wa timu hiyo Eddie Howe, Newcastle alikuwa na wachezaji wanane pekee wa akiba dhidi ya Manchester United, wakiwemo makipa wawili na vijana wawili ambao hawajawahi kucheza mechi yoyote ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Msimu huu, Newcastle wamefunga mabao 19 katika mechi 19 za Premier League, huku mfungaji bora Wilson akifunga mabao sita kati ya hayo, huku Saint-Maximin mwenye umri wa miaka 24 akiwa na mabao manne ya ligi.

Mechi kumi na tano za ligi kuu zilifutwa mwezi huu, zikiwemo Arsenal dhidi ya Wolves na Leeds na Aston Villa, ambazo zote zilikuwa zimeratibiwa kuchezwa Disemba 28.