Wednesday , 1st Jun , 2022

Mchezo mmoja wa kundi D wa ufunguzi wa Michuano ya UEFA Nations League msimu wa 2022-23 utapigwa majira ya 3:45 usiku wa leo jumatano June 01, ambapo Gareth Bale atakiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Wales wakiwa ugenini dhidi ya Poland inayoongozwa na nahodha Robert Lewandowski.

Gareth Bale na Aaron Ramsey wakishangilia goli - Wales

  (Sergio Ramos wa Hispania akihuzunika (kushoto), Cristiano Ronaldo wa Ureno akishangili goli (kulia)

Michezo mingine kumi ya Michuano hiyo itapigwa kesho Alhamis huku mchezo unaovuta hisia za wengi ni ule utakao wakutanisha Timu ya Hispania dhidi ya Ureno majira saa 4 kasoro usiku wa kesho, huku mchezo kati ya Albani na Russian ukiondolewa katika ratiba ya michuano hiyo.

Baadhi ya michezo mingine itakayopigwa kesho ni Serbia dhidi ya Norway, Czech Republic dhidi ya Switzerland, Bulgaria dhidi ya Northern Marcedonia na Slovenia dhidi ya Sweden.

Michuano hii inatajwa kuwa mbadala katika kipindi amchano michuano ya kombe la dunia ilikua inafanyika baada ya kuhamia mwezi Novemba mwaka huu tofauti ilivyo fanyika miaka ya awali ambapo ilikua ikifanyika mwezi June hadi Julai.