
Wanasayansi hao wanasema kwamba dozi hiyo itakua ni bei rahisi na kwamba tayari kuna makubaliano na mzalishaji mmoja ya kutengeneza zaidi ya dozi milioni 100 wa mwaka. Mfuko unaojihusisha na kutokomeza Malaria umesema kuwa maendeleo hayo ya hivi karibuni ni hatua kubwa sana ya kuokoa maisha ya watoto.
Imechukua zaidi ya miaka 100 kugundua chanjo halisi ya Malaria inayoenezwa na mbu. Mwaka jana shirika la afya duniani liliruhusu chanjo ya kwanza iliyogunduliwa na watafiti kutoka GSK kuanza kutumika barani Afrika.
