
Deus Kaseke aliwapatia wenyeji bao lao dakika ya 11 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na kiungo Said Ndemla.
Baada ya bao hilo tuliongeza presha langoni mwa Singida lakini tulikosa utulivu wa kumalizia nafasi tulizotengeneza.
Peter Banda aliwasawazishia bao hilo kwenye dakika ya 58 muda mfupi baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Jonas Mkude akimalizia pasi ya Moses Phiri.
Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Mkude na Kibu Denis na kuwaingiza Banda na Habib Kyombo.