Wednesday , 26th Apr , 2023

Ukosefu wa maji safi na salama umetajwa kuchangia magonjwa mbalimbali ya mlipuko na yale yakuambukizwa, hali iliyowatoa ofisini watendaji wa wizara ya maji wakiongozana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo kwenda kukagua miradi ya maji inavyofanya kazi ili wananchi wayatumie.

Watumishi hao wakiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma walifika eneo la mradi wa tanki la majisafi na salama la Buigiri lililopo Wilaya ya Chamwino nakuona uhalisia wa tenki hilo ambapo limekamilika kwa asilimia 100 kwa kuwepo kwa maji yakutosha hatua iliyilopelekea kuzinduliwa rasmi kuanza kutumika kwa  kusambaza maji kwa maeneo ya Mikoa wa Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amewaambia wananchi wa eneo hilo na viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma kwamba tanki hilo hadi kukamilika na kuanza kutumika limegharimu jumla ya Shilingi Bilioni 1.21 badala ya shilingi  bilioni 2.5 hivyo kuokoa asilimia 50 ya feha iliyotakiwa kutumika na linategemea kuzalisha Lita Milioni 7.6 kwa siku ,maji ambayo yanachimbwa kutoka chini ya Ardhi na wameyapima nakujiridhisha ni salama kwa afya za binadamu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema zoezi la uzinduaji wa kisima hicho ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mkuu Mhe.Kassimu Majaliwa  kuelekea miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo ufanyika kila tarehe 26.04 ya kila mwaka.

Malengo ya kimataifa inaelekeza ifikapo mwaka 2030 upatikanaji wa maji mijini na vijijini uwe kwa asilimia 100.