Dk.Magufuli: Jemedari jembe aliyetutoka ghafla
Machi 17, 2021, ni miongoni mwa siku ambazo haziwezi kusahaulika kwa Watanzania, kwani ni usiku ambao zilitolewa taarifa zilizoacha vinywa wazi, vilio, simanzi na majonzi kwa watu wengi nchini, baada ya kutangazwa kifo cha Rais wa awamu ya tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.